China yasema inataka uhusiano wa ngazi mpya na Ujerumani
15 Februari 2026
Matangazo
Kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya China, Wang pia amemwambia Merz kwamba China inatarajia kufanya kazi na Ujerumani kuleta "ushirikiano wa kimkakati wa pande zote".
Ameongeza kuwa kwa msaada wa Ujerumani, China pia inataka kujiandaa kwa hatua inayofuata ya ushirikiano wa ngazi za juu.
Wang amethibitisha kuiunga mkono Ujerumani kuchukua jukumu kubwa zaidi katika kudumisha "uhuru wake wa kimkakati na kujitegemea na kuwa nguvu ya kuleta ushirikiano kati ya China na mataifa ya Ulaya.
Merz anaripotiwa kujiandaa kufanya ziara yake ya kwanza nchini China mwezi huu, huku suala kuu likiwa ni jinsi ya kushughulikia mahusiano ya kibiashara yanayoendelea kubadilika.