China ndio taifa linaloongoza katika matumizi ya teknolojia ya utambuzi wa sura yaani Facial Recognition. Japo teknolojia hiyo inakosolewa kuwa inaingilia faragha ya watu, lakini China yenyewe inadai kwamba mfumo huo unafuatilia mienendo na tabia za raia wake na lengo kubwa ni kuimarisha usalama.