1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China yahimiza uhusiano thabiti na Seoul licha ya "msuguano"

14 Mei 2024

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amemwambia mwenzake wa Korea Kusini kwamba nchi hizo mbili zinapaswa kuimarisha uhusiano wao licha ya "msuguano" kati yao hivi karibuni.

https://p.dw.com/p/4fokD
Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi
Waziri wa mambo ya nje wa China Wang YiPicha: Willy Kurniawan/AFP

Kwa upande wake, Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini Cho Tae-yul amesema nchi hizo zinapaswa kusimamia kwa makini uhusiano wao.

Mkutano kati ya wanadiplomasia hao umefanyika katikati ya mvutano kuhusu Taiwan na masuala mengine ya kikanda.

Soma pia: Rais wa Korea Kusini akabiliwa na mtihani mgumu uchaguzi wa bunge

Cho aliwasili Beijing jana Jumatatu, ikiwa ni safari yake ya kwanza nchini China tangu aingie madarakani mwezi Januari, na pia ni ziara ya kwanza ya waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini kwenda Beijing katika muda wa zaidi ya miaka sita.

Uhusiano kati ya China na Korea Kusini uliyumba baada ya Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol kusema mwaka uliopita kwamba kisiwa chenye utawala wa ndani cha Taiwan, ambacho China inadai kuwa ni sehemu ya himaya yake, ni "suala la kimataifa" na wala sio suala kati ya China na Taiwan.