1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na Iran

Sylvia Mwehozi
22 Mei 2024

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi, amesema Beijing itaendelea kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na Iran, kulinda maslahi ya pamoja na kufanya juhudi za kuleta amani ya kikanda na dunia nzima.

https://p.dw.com/p/4g7rl
Wang Yi
Waziri wa mambo ya nje wa China Wang YiPicha: PEDRO PARDO/AFP

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi, amesema Beijing itaendelea kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na Iran, kulinda maslahi ya pamoja na kufanya juhudi za kuleta amani ya kikanda na dunia nzima.

Wang ameyasema hayo jana katika mazungumzo yake na naibu waziri wa mambo ya nje wa Iran, Mahdi Safari, alipohudhuria mkutano wa baraza la mawaziri wa mambo ya kigeni wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai SCO.

Mwanadiplomasia huyo wa China ametumia nafasi hiyo kutoa salamu za pole kwa waziri mwenzake wa Iran, akisema nchi hiyo imeondokewa na viongozi makini na China pia imewapoteza marafiki na washirika.

Wanadiplomasia kutoka nchi washirika wa kisiasa na kiuchumi wa Iran walisimama kimya kutoa heshima kwa marehemu Rais wa Iran Ebrahim Raisi kabla ya mkutano wa jumuiya hiyo inayoongozwa na China.