1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Charles Michel yupo ziarani Ukraine

Amina Mjahid
20 Aprili 2022

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Ulaya Charles Michel anaitembelea Ukraine kwa ziara inayolenga kuonesha uungaji mkono kwa taifa hilo linakabiliwa na vita tangu Urusi ilipotuma vikosi vyake miezi miwili iliyopita.

https://p.dw.com/p/4A8Nb
Brüssel | Sitzung Europaparlament zur Ukraine | Charles Michel
Picha: Jonas Roosens/BELGA MAG/AFP/Getty Images

Michel alilakiwa mjini Kyiv na Naibu Waziri Mkuu wa Ukraine, Olga Stefanishyna, na anatarajiwa kukutana na Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine baadaye leo. 

Ziara ya kiongozi huyo wa Umoja wa Ulaya inafanyika wakati serikali ya Ukraine imetangaza kufikia makubaliano na Urusi ya kufungua ujia mpya wa kuruhusu wanawake, watoto na wazee kuondoka kutoka katika mji uliozingirwa wa Mariupol.

soma zaidi: Mataifa ya Magharibi yaahidi msaada zaidi kwa Ukraine

Mamlaka za mji huo zinasema maelfu ya watu wameuwawa tangu kuingia kwa vikosi vya Urusi na sehemu kubwa ya majengo na miundombinu kwenye mji huo wa mwambao wa Bahari ya Azov vimeharibiwa.

Chanzo: afp