Champions League nafasi 4 tu zimebakia | Michezo | DW | 10.12.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Champions League nafasi 4 tu zimebakia

Timu saba zinawania nafasi 4 kuingia katika awamu ya mtoano ya timu 16, Liverpool, Tottenham na PSG zote mashakani

Ligi  ya  mabingwa   barani  Ulaya  Champions League, mchezo  wa  mwisho  katika  awamu  ya  makundi  unafanyika  Jumanne  na  Jumatano, ambapo wakati  Tottenham  ikiwa  katika nafasi  salama  katika  Premier League  nchini  England, inakabiliwa na  mchezo  wa  mwisho  wa  kuamua  iwapo  itabakia  katika kinyang'anyiro  hicho  katika timu 16 bora ama  la  kwa  kupambana  na Barcelona  kesho  Jumanne.

Fussball Champions League Spieltag 5 Gruppe E l Fc Bayern vs Benfica Tor 4:0 - Lewandowski (Reuters/M. Dalder)

Wachezaji wa Bayern Munich wakifurahia bao

Kocha Mauricio Pochettino  anapaswa kupata  njia kuishinda  Barcelona  na  kufikia  awamu  ya  mtoano lakini anaendelea  kuwa  na  matumaini  ya  kibarua  hicho  kigumu katika  uwanja  wa  Camp Nou kukabiliana  na  mabingwa  hao  mara tano  wa  Ulaya.

Liverpool  kwa  mara  nyingine  tena  wanalazimika  kuutegemea uwanja  wao  wa  nyumbani  wa  Anfield  kuweza  kuipa  Napoli kipigo  chake  cha  kwanza  katika  Champions League  msimu  huu, iwapo  wataweza  kuepuka  mfadhaiko  wa  kuaga  katika  awamu ya  makundi  kiasi  ya  miezi  sita  tangu  kushiriki  katika  fainali  ya msimu  uliopita  ya  Champions  League.

Fussball Champions League Spieltag 5 Gruppe C l Paris PSG vs Liverpool (Reuters/A. Boyers)

Mchezaji wa kati Draxler na mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane wakipambana

Nafasi 12  tayari zimekwisha  thibitishwa katika  awamu  ya  mtoano ambapo vilabu saba  vinapambana  kupata  nafasi  nne  zilizobaki katika  mchezo huu  wa  mwisho.

 

Mwandishi: Sekione  Kitojo / ape / dpae / rtre / afpe

Mhariri:  Yusuf Saumu