CAIRO: Condoleezza Rice ziarani nchini Misri
16 Oktoba 2007Matangazo
Waziri wa Nje wa Marekani,Condoleezza Rice akiendelea na ziara yake ya Mashariki ya Kati kupigia debe mkutano wa mwezi Novemba,amewasili Cairo nchini Misri kuzungumza na Rais Hosni Mubarak.Baada ya majadiliano yake nchini Israel na katika Ukingo wa Magharibi,Bibi Rice alitoa mwito kwa pande zote mbili kuafikiana kabla ya mkutano wa amani wa Novemba,ambao unadhamaniwa na Marekani.