1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken azungumza na marais Tshisekedi na Kagame

7 Novemba 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na kwa nyakati tofauti na rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi na yule wa Rwanda Paul Kagame.

https://p.dw.com/p/4YVek
Japan Tokyo - Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony BlinkenPicha: Jonathan Ernst/Reuters/AP/picture alliance

Kulingana na msemaji wa serikali ya Washington Matthew Miller, Blinken amezungumza na viongozi hao wawili kuhusu hali tete ya kiusalama na mgogoro wa kibinaadamu katika mpaka wao wa pamoja huku akipendekeza mvutano kati ya Kinshasa na Kigali, utatuliwe kwa njia za kidiplomasia.

Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Marekani amezihimiza Kongo na Rwanda kuchukua hatua za kupunguza mzozo huo hasa kwa kuwaondoa wanajeshi kwenye eneo la mpakani.