1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSaudi Arabia

Blinken akutana na Mwanamfalme wa Saudi Arabia

7 Juni 2023

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Antony Blinken amekutana leo na mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia mwanamfalme Mohammed Salman kwenye mji wa mwambao wa Jeddah.

https://p.dw.com/p/4SI8I
FILE PHOTO: Saudi Crown Prince Mohammed bin Salman receives U.S. President Joe Biden at Al Salman Palace upon his arrival in Jeddah
Mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia mwanamfalme Mohammed Salman akimkaribisha Rais Joe Biden mjini Jeddah.Picha: Bandar Algaloud/REUTERS

Wawili hao wamezungumzia masuala kadhaa ikiwemo rikodi dhaifu ya haki za binadamu kwenye taifa hilo la ghuba.

Afisa mmoja wa Marekani amesema mazungumzo baina ya viongozi hao wawili yaliyodumu kwa zaidi ya dakika 40 yalikuwa ya uwazi na yalilenga kuimarisha mahusiano yanayolegalega kati ya Washington na Riyadh.

Blinken anafanya ziara ya siku tatu kwenye ufalme huo wenye utajiri mkubwa wa mafuta katika wakati Marekani inatiwa wasiwasi na maamuzi ya hivi karibuni ya Saudia ikiwemo kujongeleana na Iran.

Akiwa nchini humo Blinken atajaribu kutafuta majibu juu ya mizozo nchini Sudan na Yemen, mshikamano wa kulishinda kundi la itikadi kali linalojiita dola la kiislamu na mahusiano baina ya mataifa ya kiarabu na Israel.