Blatter: Ni ″kosa″ Qatar kuandaa Kombe la Dunia 2022 | Michezo | DW | 16.05.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Blatter: Ni "kosa" Qatar kuandaa Kombe la Dunia 2022

Rais wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni – FIFA Sepp Blatter amesema ilikuwa kosa kuichagua Qatar kuandaa dimba la Kombe la Dunia mwaka wa 2022 kwa sababu ya hali ya joto kali nchini humo

Blatter amekiambia kituo kimoja cha televisheni nchini Uswisi kuwa, na namnukuu “unajua, kila mmoja hufanya makosa maishani”.

Kiwango cha wastani cha joto ni nyuzijoto 40 katika miezi ya Juni na Julai, kipindi ambacho tamasha la kombe la dunia hupangwa kufanyika. Blatter amesema kuna uwezekano mkubwa kuwa dimba hilo la mwaka wa 2022 litaandaliwa katika msimu wa baridi. Wakati huo, kiwango cha joto hufikia nyuzijoto 25.

Hata hivyo rais huyo wa FIFA hakuzungumza lolote kuhusu madai ya rushwa kuhusiana na mchakato wa kupiga kura uliosababisha Qatar kuchaguliwa kuandaa kombe la dunia mwaka 2022. Hata hivyo alisema kulikuwa na shinikizo kubwa la kisiasa kutoka Ufaransa na Ujerumani.

Maandamano Brazil

Maandamano ya kupinga maandalizi ya Dimba la Kombe la Dunia nchini Brazil

Maandamano ya kupinga maandalizi ya Dimba la Kombe la Dunia nchini Brazil

Wakati huo huo, Brazil inakabiliwa na mtihani wa maandalizi yake ya usalama kwa ajili ya michuano ya dimba la Kombe la Dunia. Wananchi wanaokasirishwa na gharama kubwa za kuandaa michuano hiyo wiki hii walifanya maandamano ya kupinga gharama zinazotumiwa katika maandalizi ya tamasha hilo pamoja na migomo ya wafanyakazi katika miji kadhaa mikubwa nchini humo.

Maelfu ya walimu waliandamana katika mji wa Sao Paulo takriban kwa wiki nane sasa wakidai kulipwa mishahara mizuri na kuwepo kwa mazingira mazuri ya kazi. Migomo ya kazi inayoendelea kufanywa na walimu hao na polisi na tishio la kufanyika kwa mgomo wa taifa zima na polisi pia inazusha hofu ya vurugu ikiwa zimebakia wiki nne tu kabla ya kuanza kwa michuano ya soka Kombe la Dunia.

Jumla ya watu 10,000 wamendamana katika mitaa ya mji wa Belo Horizonte, Barasilia mji mkuu wa Brazil, Manaus, Porto Alegrea, Rio na Sao Paulo. Katika mji mkuu wa kibiashara wa Sao Paulo takriban wanachama 5,000 wa Vugugu la Wafanyakazi wasiokuwa na Makaazi waliwasha matairi ya magari na kuandamana hadi katika uwanja wa Corinthians Arena ambapo ndipo patakapofanyika pambano la ufunguzi kati ya Brazil na Coatia hapo Juni 12. Huyu hapa mmoja wa waandamanaji

Mwandishi: Bruce Amani/DPA/AFP/Reuters
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman