1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden na Trump washinda michujo yao Michigan

John Juma
28 Februari 2024

Rais wa Marekani Joe Biden ameshinda kwa urahisi uchaguzi wa mchujo wa chama cha Demokratic kwenye jimbo la Michigan jana Jumanne.

https://p.dw.com/p/4czYB
 Joe Biden v Donald Trump
Joe Biden na Donald Trump mwaka 2022

Rais wa Marekani Joe Biden ameshinda kwa urahisi uchaguzi wa mchujo wa chama cha Demokratic kwenye jimbo la Michigan jana Jumanne.

Hata hivyo katika jimbo hilo lenye wakaazi wengi wamarekani wenye asili ya Kiarabu, kiwango cha wademokrats walioonesha kukipinga chama hicho kupitia kura zao, kutokana na msimamo wake wa kuunga mkono vita vya Israel katika Ukanda wa Gaza dhidi ya Hamas  kilipindukia matarajio ya waandaaji wa mchakato huo.

Soma: Biden na Trump washinda chaguzi za awali Michigan

Rais wa zamani Donald Trump wa Republican vilevile alishinda mchujo huo wa Michigan kwa kura nyingi dhidi ya mshindani wake Nikki Haley.

Ingawa Biden na Trump walitarajiwa kushinda kwa urahisi michujo hiyo, idadi ya kura walizopata zinaangaliwa kwa karibu kama dalili za kuyumba kwa uungwaji mkono wao.