1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMarekani

Biden azirai Misri na Qatar zishinikize kuachiwa mateka

6 Aprili 2024

Rais Joe Biden wa Marekani amewaandikia barua viongozi wa Misri na Qatar akiwatolea mwito wa kulishinikiza kundi la Hamas kufikia makubaliano na Israel ya kuwaachia huru mateka inaowashikilia.

https://p.dw.com/p/4eURk
Rais Joe Biden wa Marekani
Rais Joe Biden wa MarekaniPicha: Darryl Webb/AP/picture alliance

Hayo yameripotiwa na shirika la habari la Associated Press likimnukuu afisa mmoja wa ngazi juu wa utawala mjini Washington.

Afisa huyo ambaye amezungumza kwa sharti la kutotajwa jina amesema barua za Biden kwenda kwa rais Abdel Fattah el-Sissi wa Misri na Mtawala wa Qatar  Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani ni sehemu ya juhudi za Marekani za kufanikisha kupatikana makubaliano ya kusitisha mapigano kwenye Ukanda wa Gaza.

Zimetumwa katika wakati mkuu wa shirika la ujasusi la Marekani CIA, William Burns atakuwa mjini Cairo leo Jumamosi na kesho Jumapili kwa mashauriano kuhusu kuachiwa mateka wa Israel.

Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Israel la Mosad, David Barnea naye pia atahudhuria mazungumzo hayo ya nchi Misri.