1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Daktari wa Biden asema yuko imara kutekeleza majukumu yake

Bruce Amani
29 Februari 2024

Daktari wa Rais wa Marekani Joe Biden amesema kuwa kiongozi huyo yuko katika hali nzuri kuongoza na hakuna wasiwasi wowote wa kiafya.

https://p.dw.com/p/4d0fD
Marekani | Rais Biden wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Michigan
Rais Biden akiwa katika kampeni jimboni MichiganPicha: Evan Vucci/AP/picture alliance

Hii ni baada ya rais huyo mwenye umri wa miaka 81 kufanyiwa uchunguzi wa mwisho wa matibabu kabla ya uchaguzi Biden na Trump washinda michujo yao Michigan huku umri wake ukionekana kuwa suala muhimu.

Ripoti hiyo ya uchunguzi wa kila mwaka iliyosubiriwa kwa hamu katika hospitali ya kijeshi ya Walter Reed nje ya mji wa Washington imetolewa wiki chache tu baada ya ripoti ya mwanasheria maalum kumuonyesha kuwa ni mzee na msahaulifu.

Soma pia: Madaktari: Afya ya Biden ni njema

Daktari Kevin O'Connor amesema Biden anaendelea kutekeleza majukumu yake bila matatizo yoyote. Kuna uwezekano mkubwa kuwa Biden atapambana kwa mara nyingine na Donald Trump mwenye umri wa miaka 77 katika uchaguzi wa Novemba.