1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Biden aonyesha matumaini ya kusitisha mapigano Gaza

Amina Mjahid
27 Februari 2024

Rais wa Marekani Joe Biden amesema ana matumaini kwamba hatua ya kusitisha mapigano mjini Gaza, huenda ikafikiwa mwanzoni mwa wiki ijayo.

https://p.dw.com/p/4cvS2
Marekani| Rais Joe Biden mjini New York
Rais Biden amesema vita vinaweza kusitisha mpaka mwisho wa mwezi wa RamadhaniPicha: Jim Watson/AFP/Getty Images

Kwa mujibu wa Biden, Israel iko tayari kusitisha operesheni zake wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kama sehemu ya mpango wowote utakaofikiwa. Alipoulizwa wakati wa kampeni zake za uchaguzi mjini New York, ni lini hasa mpango huo utakapoanza kutekelezwa, Biden alisema huenda mpango huo ukafikiwa Jumatatu wiki ijayo.

"Natumai mwanzoni mwa mwisho wa juma hili. Mwishoni mwa juma hili. Mshauri wangu wa masuala ya usalama wa taifa ameniambia kwamba tuko karibu, tuko karibu. Lakini bado hatujamaliza, matumaini yangi ni kwamba wiki ijayo Jumatatu tutakuwa na makubaliano ya kusitisha mapigano. Natumai hilo litafanyika mwishoni mwa juKiKiongozi wa Hamas awasili Cairo kujadili hali ya Gazaongozi wa Hamas awasili Cairo kujadili hali ya Gazama," alisema Biden.

Soma pia: Kiongozi wa Hamas asema mkataba wa amani lazima umalize vita

Hata hivyo, maafisa wa kundi la wanamgambo la Hamas wameliambia shirika la habari la Reuters kwamba matamshi ya Biden hayaendani na kile kinachoendelea katika uwanja wa mapigano.

Kufuatia hali ya kibinaadamu kuzidi kuwa mbaya mjini Gaza, wawakilishi kutoka Misri, Qatar, Marekani, Ufaransa na mataifa mengine wamekuwa wakijadiliana namna ya kusitisha vita kati ya pande mbili hasimu Israel na Hamas na kuachiwa kwa mateka wanaoshikiliwa mjini Gaza.