1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden akataa kuzungumzia mashitaka dhidi ya Trump

31 Machi 2023

Rais wa Marekani Joe Biden leo amekataa kutoa tamko lolote kuhusiana na kufunguliwa mashtaka kwa mtangulizi wake Donald Trump

https://p.dw.com/p/4PZAZ
USA, New York | Nachdem eine Grand Jury für die Anklage von Donald Trump gestimmt hat
Picha: Selcuk Acar/AA/picture alliance

Trump anakuwa rais wa kwanza wa zamani nchini humo kukabiliwa na mashtaka ya jinai. Biden aliyekuwa anaelekea Mississippi kutoka Ikulu ya Marekani, White House, kwa makusudi hakuyajibu maswali aliyoulizwa na waandishi habari kuhusu suala hilo.

Trump anayeonekana kama mgombea aliye katika mstari wa mbele katika kuwania urais kwa tiketi ya chama cha Republican mwaka 2024, ameikosoa hatua hiyo ya kumfungulia mashtaka akisema ni "hujuma za kisiasa na kutatiza uchaguzi" kutoka kwa waendesha mashtaka na wapinzani wake wa chama cha Democratic.