Barcelona wafufuka, Madrid hoi | Michezo | DW | 26.08.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Barcelona wafufuka, Madrid hoi

Uhispania kulirindima mechi za La Liga ambapo baada ya kipigo kwenye mechi yao ya kwanza, mabingwa Barcelona walijitahidi na kuwalaza Real Betis magoli matano kwa mawili uwanjani Camp Nou.

Lionel Messi, Luis Suarez na Ousmane Dembele hawakuwepo kwenye mechi hiyo ila Antoine Griezmann aliitumia fursa hiyo vyema na kufunga mabao mawili kisha mengine yakafungwa na Jordi Alba, Arturo Vidal na Perez.

Real Madrid walilazimishwa sare ya goli moja walipokuwa wakicheza na Real Valladolid ambapo Karim Benzema alifunga goli la ufunguzi ila Guardiola alisawazisha na kuwapelekea kugawanya alama.

Atletico Madrid walipata ushindi mwembamba wa bao moja lililopachikwa wavuni na Vitolo baada ya kuandaliwa pasi safi kabisa na Joao Felix.