Barcelona hoi, Madrid washinda mechi ya kwanza La Liga | Michezo | DW | 19.08.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Barcelona hoi, Madrid washinda mechi ya kwanza La Liga

Ligi Kuu ya Uhispania La Liga ilianza Ijumaa na Barcelona walianza kwa mguu mbaya baada ya kulazwa moja bila na Athletic Bilbao. Aritz Aduriz ndiye aliyekuwa mwiba kwao katika mechi hiyo waliyoicheza ugenini.

Aduriz aliyeingia katika dakika za lala salama alipachika wavuni goli maridadi dakika moja kabla muda wa ziada kuisha na kuyadidimiza matumaini ya Barca kutoka angalau na pointi moja katika mechi ambayo Lionel Messi hakushiriki kwa kuwa hakuwa imara kulingana na kocha Ernesto Valverde.

Real Madrid nao walikuwa washindi wa 3-1 walipokuwa wakichuana na Celta Vigo Gareth Bale ndiye aliyekuwa nyota kwenye mechi hiyo na sasa kocha wake Zinedine Zidane amebadilisha msimamo wake kumuhusu na anasema kuwa raia huyo wa Wales hatoihama tena Madrid.

"Mimi na yeye tulizungumza kabla mechi Nimesema mara mbili au tatu kwamba atasalia hapa na wachezaji wote wanafikiria tu kuhusu msimu ulio mbele yetu. Nafikiri Gareth na kila mmoja walicheza vizuri sana na yeye pamoja na kila mtu wanafikiria kusalia hapa na kuwa na msimu mzuri," alisema Zidane.

Kabla kuanza kwa msimu Bale aliripotiwa kukaribia kujiunga na klabu ya nchini China Jiangsu Suning.