Bangladesh imetangaza kufanya Uchaguzi Mkuu Februari 12
11 Desemba 2025
Matangazo
Maandamano hayo ya mwaka uliopita, yaliyouondoa utawala wa Waziri Mkuu wa zamani Sheikh Hasina.
Kamishna wa Tume hiyo Nasir Uddin, amesema kura ya maoni kuhusu mfumo wa utawala wa demokrasia pia itafanyika siku hiyo.
Nchi hiyo ya kiislamu iliyo na idadi ya watu milioni 170 barani Asia, ilitumbukia katika mgogoro wa kisiasa tangu Hasina alipoondolewa madarakani mwezi Agosti mwaka 2024 hatua iliyomaliza utawala wake wa miaka 15 madarakani.
Chama chake cha Awami League kimepigwa marufuku kushiriki uchaguzi huo.
Kiongozi wa mpito ambaye aliwahi kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel Muhammad Yunus, aliyerejea nyumbani kutoka Uhamishoni mwezi Agosti mwaka jana kuiongoza serikali hiyo ataachia madaraka baada ya uchaguzi huo.