Ban Ki Moon amtaka Gadaffi asitishe mashambulio | Habari za Ulimwengu | DW | 07.03.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ban Ki Moon amtaka Gadaffi asitishe mashambulio

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon,amemtaka kiongozi wa Libya,Kanali Muammar Gaddafi,asitishe vitendo vyote vya kuwashambulia raia wa kawaida.

default

Ban Ki-moon,Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Kwa mujibu wa afisi yake ya mawasiliano,uongozi wa Libya huenda ukalazimika kuwajibika endapo utazikiuka sheria za kimataifa.Ili kuiweka sawa Libya,Ban Ki Moon amemteua waziri wa mambo ya nje wa Jordan wa zamani,Abdelilah Al-Khatib kuwa mjumbe maalum atakayeushawishi uongozi wa Libya kukaa katika meza ya mazungumzo ya dharura.

Azma ya mazungumzo hayo ni kulitafutia suluhu tatizo la wakimbizi wanaoyakimbia machafuko nchini humo. 

Flash-Galerie Rebellen in Libyen

Wapiganaji wanaompinga Kanali Gaddafi:Miji ya Misrata,Zawiya na Ras Lanuf inadhibitiwa na waasi

Pindi waziri wa mambo ya nje wa Libya alipoiridhia mipango hiyo,Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa una mpango wa kuipelekea kundi maalum la wataalam watakaoitathmini hali halisi na mahitaji yake.Wakati huohuo,kuna hofu kuwa Libya huenda ikaingia katika kipindi cha vita vya wenyewe kwa wenyewe.Mapigano makali yameripotiwa kutokea pale vikosi vinavyomuunga mkono Kanali Muammar Gaddafi vilipojaribu kuiteka nyara miji ya Misrata,Az-Zawiya na Ras Lanuf inayodhibitiwa na waasi kwa sasa.

DW inapendekeza

 • Tarehe 07.03.2011
 • Mwandishi Thelma Mwadzaya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/10UQG
 • Tarehe 07.03.2011
 • Mwandishi Thelma Mwadzaya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/10UQG

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com