BAGHDAD: Kipaumbele ni kuimarisha usalama Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 10.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Kipaumbele ni kuimarisha usalama Iraq

Makamu wa Rais wa Marekani,Dick Cheney amekutana na Waziri Mkuu wa Iraq Nouri al-Maliki na viongozi wengine alipofanya ziara ya ghafula katika mji mkuu wa Iraq,Baghdad.Baada ya mkutano huo,Al-Maliki aliwaambia waandishi wa habari kuwa majadiliano yao yalihusika na usalama na masuala mengine ya ndani.Wakati huo huo Cheney amesema viongozi hao wamekubaliana kuwa kipaumbele ni kuimarisha usalama nchini Iraq.Makamu wa rais Cheney pia ametumia fursa ya mkutano huo kuwasihi wabunge wa Iraq kutokwenda katika likizo ya majira ya joto.Wabunge hao walipanga kwenda mapumzikoni kwa miezi miwili.Iraq ni kituo cha mwanzo cha ziara ya Cheney inayompeleka pia Umoja wa Falme za Kiarabu,Saudi Arabia,Misri na Jordan.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com