1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiAfrika

Awamu ya tano ya kufukuliwa miili katika msitu wa Shakahola

4 Juni 2024

Miili saba imefukuliwa msituni shakahola kwenye awamu ya tano ya kufukua makaburi ya wahanga wa kadhia ya mhubiri Paul Mackenzie,

https://p.dw.com/p/4gcjO
Kenya | Wahudumu wa afya wakiuingiza chumba cha maiti mwili wa muathirika wa mkasa wa shakahola.
Wahudumu wa afya wakiuingiza chumba cha maiti mwili wa muathirika wa mkasa wa shakahola huko Kenya.Picha: Luis Tato/AFP/Getty Images

Awamu hiyo ya tano ilianza tena mapema wiki hii na waziri wa usalama nchini Kenya Kithure Kindiki. Kufikia sasa idadi ya miili iliyofukuliwa kwa jumla imefikia 436. 

Makaburi mengine 50 yamepatikana na shughuli ya kufukuwa inaendelea. Daktari Mkuu wa Serikali, Johansen Oduor, ameeleza kuwa miili hiyo saba imepatikana kwenye makaburi manne, huku miili minne ikipatikana imezikwa kwenye kaburi moja.

Soma pia:Miili ya wahanga wa Shakahola yatolewa kwa familia Kenya

Daktari Oduor ameeleza pia kuwa makaburi hayo yametambuliwa kwa urahisi kutokana na udongo kuwa  mwepesi. 

Paul Mackenzie, mhubiri aliyekamatwa kwa madai ya kuwalazimisha wafuasi wake kujizuia kula na kunywa hadi kufa pamoja na washukiwa wengine 94 ambao bado wanazuiliwa katika gereza la shimo la tewa mjini Mombasa.