1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Australia yavunja mtandao wa 'kishetani' dhidi ya watoto

1 Desemba 2025

Polisi Australia wamekamata washukiwa wanne wa kadhia ya 'kishetani' wanaohusishwa na unyanyasaji wa watoto kingono.

https://p.dw.com/p/54Xpi
Polisi wa Australia mjini Sydney 2017
Polisi Australia wafichua mtandao wa dhuluma ya 'kishetani' inayohusisha unyanyasaji wa watoto kingonoPicha: picture alliance/Photoshot/picture alliance

Polisi nchini Australia imesema siku ya Jumatatu kuwa imewashitaki watu wanne mjini Sydney, wanaoshukiwa kuwa sehemu ya mtandao wa kimataifa unaosambaza kile ilichokiita maudhui ya ‘kishetani' ya unyanyasaji wa watoto kingono.

Kulingana na taarifa ya polisi jimbo la New South Wales, maafisa wao waliwakamata watuhumiwa hao baada ya kuchunguza kadhia hiyo ya kimataifa dhidi ya watoto.

Wakati wa uchunguzi, wapelelezi walifichua mtandao wa wanyanyasaji watoto kingono wanaohusika pakubwa katika kumiliki, kusambaza na kuwezesha uwepo wa maudhui hayo kwenye tovuti inayosimamiwa kimataifa.