SiasaIran
Araghchi 'Hakuna mawasiliano ya moja kwa moja na Witkoff'
17 Machi 2026
Matangazo
Kauli yake inatofautiana na taarifa za awali za vyombo vya habari kwamba kumekuwepo na mawasiliano baina yao katika siku za karibuni.
Araghchi amesema kupitia mtandao wa X kwamba, mara ya mwisho aliwasiliana na Witkoff kabla ya uamuzi wa Rais Donald Trump wa kukatisha mchakato wa kidiplomasia na kuanzisha operesheni nyingine haramu ya kijeshi.
Gazeti la Marekani la Axios na vyombo vingine vya habari viliripoti juu ya kuwepo kwa mawasiliano ya moja kwa moja kati ya Witkoff na Araghchi hivi karibuni, vikiwanukuu afisa wa Marekani na Iran na duru zenye ufahamu na suala hilo waliosema Araghchi alimtumia ujumbe Witkoff.