1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaYemen

Al-Qaeda nchini Yemen yatangaza kifo cha kiongozi wake

Sudi Mnette
11 Machi 2024

Tawi la Al-Qaeda nchini Yemen limetangaza kifo cha kiongozi wake Khalid Batarfi na kumtaja mrithi wake, Saad bin Atef al-Awlaki. Shirika la Ujasusi la SITE liliripoti jana Jumapili.

https://p.dw.com/p/4dMy1
Kiongozi wa Al-Qaeda kwa Yemen Khalid Batarfi
Kiongozi wa tawili la Al-Qaeda kwa Yemen aliyetangazwa kufariki dunia, Khalid BatarfiPicha: ZumaPress/picture alliance

Shirika hilo limeandika mwili wa Batarfi ulionyeshwa katika picha zilizotolewa na Al-Qaeda katika Rasi ya Uarabuni (AQAP) ukiwa kwenye sanda ya maziko na ukiwa umefungwa kwenye bendera yenye jina la kundi hilo la kijihadi.

Hakukuwa na maelezo ya kina kuhusu muda wa kifo hicho wala sababu. Lakini inaaminika alikuwa na umri wa katika miaka ya 40. Mapema Februari 2020, AQAP ilimtangaza Batarfi kuwa ameteuliwa kuwa kiongozi wake, kufuatia kifo cha mtangulizi wake, Qassim al-Rimi, katika shambulio la droni.

SITE imesema kundi hilo limemtaja Saad bin Atef al-Awlaki, kama kiongozi wakempyaambaye mara ya mwisho alionekana kwenye video iliyotolewa Februari 2023 akiwataka watu wa madhehebu ya Sunni kujiunga na AQAP.