Ajali ya boti yawauwa watu 43 kwenye pwani ya Libya | Matukio ya Afrika | DW | 21.01.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Ajali ya boti yawauwa watu 43 kwenye pwani ya Libya

Wahamiaji wasiopungua 43 kutoka magharibi ya Afrika wamekufa katika ajali ya boti ya mpira iliyotokea nje kidogo ya pwani Libya jana Jumatano.

Hayo ni kulingana na mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa yanayoshughulikia wakimbizi na uhamiaji ambayo pia yamesema wahamiaji wengi 10 wameokolewa.

Mashirika hayo yamearifu kuwa ajali hiyo ya boti ambayo ni kwanza kuripotiwa tangu kuanza mwaka 2021 imefuatia hitilafu ya injini saa chache baada ya chombo hicho kuanza safari yake kutoka mji wa Zawya kuelekea Ulaya.

Manusura wa ajali hiyo ambao ni kutoka mataifa ya Côte d'Ivoire,, Nigeria, Ghana na Gambia wamesema wenzao wote waliokufa pia walikuwa wanatoka mataifa hayo ya magharibi mwa Afrika.

Libya imegeuka lango kuu la safari za wahamiaji kutoka Afrika wanaojaribu kuingia Ulaya kupitia bahari ya Mediterrania tangu kuangushwa kwa utawala wa Muammar Ghadaffi mwaka 2011.