1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika Mashariki yakumbwa na ukosefu wa mtandao wa Intaneti

13 Mei 2024

Nchi kadhaa za Afrika Mashariki zimekumbwa na ukosefu wa mtandao wa Intaneti baada ya nyaya za chini ya bahari kuharibika.

https://p.dw.com/p/4flgT
Symbobild Netzwerkkabel mit einem Knoten
Picha: Steinach/IMAGO

Shirika la uchunguzi la mtandao la NetBlocks limesema Tanzania na kisiwa cha Ufaransa cha Mayotte ndizo zilizoathirika zaidi na hitilafu hiyo ya mtandao wa Intaneti.

Kupitia ukurusa wa kijamii wa X, zamani ukijulikana kama Twitter, Netblocks imesema nyaya za mawasiliano za chini ya habari za SEACOM na EASSy zimeharibika.

Soma pia: Marekani, Uingereza zaituhumu China kwa ujasusi wa mtandaoni

Waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia wa Tanzania Nape Nnauye amesema uhabirifu katika nyaya hizo za mawasiliano umetokea kati ya Msumbiji na Afrika Kusini na kwamba upatikanaji wa huduma za Intaneti na simu za kimataifa utakuwa wa kiwango cha chini.

Msumbiji, Malawi, Burundi, Somalia, Rwanda, Uganda, Madagascar na visiwa vya Comoros pia zilikumbwa na tatizo la kukosekana kwa mtandao wa Intaneti.