1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afisa wa Kenya afariki Marekani

Tatu Karema
16 Februari 2024

Afisa mmoja wa Kenya, ambaye alikuwa nchini Marekani kwa mazungumzo kuhusu kikosi cha askari wa kimataifa kusaidia polisi ya Haiti kupambana na magenge ya wahalifu, amekutikana amekufa katika chumba chake hotelini.

https://p.dw.com/p/4cUoj
Polisi wa kuzuwia fujo nchini Kenya.
Polisi wa kuzuwia fujo nchini Kenya.Picha: James Keyi/REUTERS

Polisi ya mjini Washington ilisema siku ya Alhamis (Februari 15) kwamba Nyamato Walter, aliyekuwa na umri wa miaka 39, alikutikana akiwa hana fahamu na kuthibitishwa papo hapo kuwa amkufariki dunia.

Taarifa ya polisi haikutoa sababu ya kifo hicho, lakini ilibainisha kwamba uchunguzi unasimamiwa na kikosi maalumu chenye utaalamu wa vifo vya kawaida na vya kujitoa uhai.

Kikosi hicho cha kimataifa kinachotarajiwa kuongozwa na Kenya kimekabiliwa na vikwazo kadhaa.

Soma zaidi: Ruto: Mpango wa kutuma askari wa Kenya, Haiti unaendelea

Mnamo mwezi Januari mahakama moja ya Nairobi ilizuia pendekezo la kutumwa polisi 1,000 wa Kenya nchini Haiti, ikisema hatua hiyo ni kinyume cha katiba.

Hata hivyo, Rais William Ruto wa Kenya anasema mpango huo utaendelea.