1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfghanistan

Afghanistan yawazuia wasichana kutoendelea na shule

20 Machi 2024

Shule nchini Afghanistan zimefunguliwa kwa mwaka mpya wa masomo hii leo, huku wasichana wakilalamika kwa miaka mitatu mfululizo kuendelea kupigwa marufuku kujiunga na masomo ya sekondari.

https://p.dw.com/p/4dwi4
Afghanistan | Masomo ya wasichana
Wasichana wakihudhuria shule AfghanistanPicha: Ebrahim Noroozi/AP Photo/picture alliane

Mwezi Machi mwaka 2022, mwaka mmoja baada ya kurejea madarakani, mamlaka ya Taliban ilichukua uamuzi wa kuwazuia wasichana kuendelea na shule za sekondari, katika hatua yao yakutekeleza sheria kali ya Uislamu ambayo inapingwa na Umoja wa Mataifa inayoitaja kuwa ubaguzi wa kijinsia.

Afghanistan ndio nchi pekee duniani ambayo imepiga marufuku wasichana kuendelea na elimu mara baada ya kumaliza shule ya msingi. Vyuo vikuu vya serikali pia vilianza mwaka mpya hivi karibuni, lakini tangu Desemba mwaka 2022, wanawake wamezuiwa kuhudhuria masomo.