ABUJA : Serikali yataka mahkama imtimuwe makamo rais | Habari za Ulimwengu | DW | 28.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ABUJA : Serikali yataka mahkama imtimuwe makamo rais

Serikali ya Nigeria hapo jana iliwasilisha mahkamani kesi ya madai inayotaka kutangazwa kwamba Atiku Abubakar hana tena sifa za kuendelea kuwa Makamo wa Rais wa nchi hiyo tokea akiasi chama tawala cha PDP.

Abubakar ambaye kwa miezi kadhaa amekuwa kwenye mzozo mkali na Rais Olesegun Obasdanjo wiki iliopita alikitelekeza chama cha PDP kwa kuchaguliwa kuwa mgombea wa urais wa chama kikuu cha upinzani cha Action Congress AC katika uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika mwaka 2007.

Waziri wa sheria wa Nigeria Bayo Ojo ameiomba Mahkama ya Rufaa itangaze kwamba kwa mujibu wa sheria ya Nigeria na katika kuhakikisha kwamba ofisi ya rais inaendesha shughuli zake kwa ufanisi rais na makamo wake lazima wakuweko ndani ya chama kimoja.

Obasanjo alimtimuwa Abubakar kwenye wadhifa wake hapo Jumamosi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com