ABUJA : Obasanjo hana madaraka kumuondowa makamo rais | Habari za Ulimwengu | DW | 20.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ABUJA : Obasanjo hana madaraka kumuondowa makamo rais

Mahkama ya Nigeria imepitisha hukumu leo hii kwamba Rais Olesegun Obasanjo alikuwa hana madaraka ya kumuondowa makamo wa rais na hiyo kuweka hai matumaini ya Atiku Abubakar ya kugombania uchaguzi wa urais hapo mwezi wa April.

Uamuzi huo ni uhai wa kisiasa kwa Abubakar ambaye anakabiliwa na tuhuma za rushwa kwa sababu ina maanisha kwamba kwa kuendelea kushikilia wadhifa wa makamo wa rais anaendelea kuwa na kinga ya kikatiba ya kutoshtakiwa akielekea kipindi hicho cha uchaguzi.

Msemaji wa Obasanjo ametangaza nafasi ya makamo wa rais kuwa wazi hapo mwezi wa Desemba kwa hoja kwamba Abubakar alikuwa amejiuzulu kiutaratibu kwa kujiunga na chama cha upinzani cha Action ili aweze kugombania urais.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com