Zoezi la kuhesabu kura linaendelea nchini Cote D'Ivoire baada ya uchaguzi wa bunge , ukiwa wa kwanza baada ya kuondolewa madarakani rais Laurent Gbagbo.
Gazeti la serikali la Uhispania la El Pais, limesema nchi hiyo itatuma idadi ndogo ya mfumo wa ulinzi wa angani aina ya Patriot kwa Ukraine.
Mamlaka ya Burkina Faso imesema imesimamisha kwa wiki mbili matangazo ya BBC na VOA baada ya kuiangazia ripoti iliyodai jeshi la nchi hiyo linatekeleza mauaji ya kiholela.
Serikali ya Misri imepeleka ujumbe Israel kwa matumaini ya kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano na wanamgambo wa kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza.