Deutsche Welle: Kwa uchache watu wanane wahofiwa kufariki dunia na wengi zaidi hawajuilikani walipo kufuatia ajali ya boti kwenye kisiwa cha Lamu nchini Kenya.
Ripoti ya mashirika ya haki za binadamu imeeleza kuwa jumla ya watu 118 walikuwa wahanga wa mauaji ya kiholela yaliyofanywa na polisi Kenya mwaka uliopita na kulaani hali ya kutowajibishwa kwa maafisa hao nchini humo.
Miili ya watu wasiopungua 13 imeopolewa kutoka maeneo tofauti ya mji mkuu wa Kenya, Nairobi baada mafuriko ya kutisha kulikumba taifa hilo la Afrika Mashariki.
Kuanzia kaskazini hadi kusini, nchi nyingi barani Afrika zimeathiriwa na athari za mabadiliko ya hali ya hewa. Ukame uliokithiri, mafuriko na hali ya kuongezeka kwa joto. Malawi, Kenya na Mali pia hivi karibuni zimekabiliwa na majanga yanayohusiana na hali ya hewa.