1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky ahimiza msaada zaidi kwa ukraine, mkutano wa Munich

17 Februari 2024

Rais wa Ukraine VVolodymyr Zelensky hii leo amewatolea mwito washirika wa nchi yake kuongeza uungaji mkono katika vita vyake dhidi ya uvamizi wa Urusi.

https://p.dw.com/p/4cWOR
Munich, Ujerumani | Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy akihutubia katika mkutano wa usalama
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy akihutubia katika mkutano wa usalama wa Munich nchini UjerumaniPicha: Wolfgang Rattay/REUTERS

Zelesnky ameyasema hayo katika hotuba yake kwenye mkutano wa kimaitaifa kila mwaka wa masuala ya usalama wa Munich ambao unawaleta pamoja maafisa wa ngazi za juu wa ulinzi na wanasiasa wa haiba ya juu kujadili sera na hatua za kimataifa kuhusu ulinzi na usalama.

Zelensky amesema iwapo hatua hazitachukuliwa kwa wakati huu miaka michache baadae rais wa Urusi Vladimir Putin atabadilisha hali kuwa janga la kutisha.

Soma pia:Viongozi wa dunia kujadili usalama katika mkutano wa Kimataifa wa Munich

Kauli ya Zelensky inakuja baada ya hotuba ya kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, ambaye alitoa wito kwa washirika wa Ukraine ndani ya Umoja wa Ulaya kuiga mfano wa serikali mjini Berlin na kuongeza misaada kwa Ukraine, akisema ni wakati mwafaka wa kuimarisha usalama wa Ulaya.

Msaada wa kijeshi wa Ujerumani kwa Ukraine umefikia kiasi cha dola bilioni 7.5, huku ahadi za miaka ijayo zikiwa na jumla ya dola bilioni 6.