1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan Kusini

Zaidi ya watu milioni 7 kukabiliwa na njaa Sudan Kusini

1 Mei 2024

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO, limesema zaidi ya watu milioni 7 Sudan Kusini wanatarajiwa kukabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula kuanzia sasa hadi mwezi wa Julai.

https://p.dw.com/p/4fOdY
Watu zaidi ya milioni 7 kukabiliwa na kiwango cha juu cha njaa Sudan Kusini
Watu zaidi ya milioni 7 kukabiliwa na kiwango cha juu cha njaa Sudan KusiniPicha: Dominika Zarzycka/NurPhoto/picture alliance

Shirika la FAO limesema kiwango cha juu zaidi cha njaa cha asilimia 65 na 75 ya idadi jumla ya watu kinaripotiwa katika jimbo la kaskazini la Unity, Upper Nile, Jonglei na pia kwenye mkoa wa mashariki mwa Sudan Kusini wa Pibor karibu na mpaka na Ethiopia na miongoni pia mwa raia wa Sudan Kusini wanaorejea nyumbani kutoka nchi inayokabiliwa na vita ya Sudan.

Shirika hilo la chakula na kilimo limesema sababu zinazopelekea usalama mdogo wa chakula nchini humo ni changamoto za kiuchumi zilizosababisha viwango vya juu vya mfumuko wa bei, usambazaji mdogo wa chakula, mafuriko na migogoro

Sudan Kusini nchi changa kabisa duniani, iliyopata uhuru wake kutoka Sudan mwaka 2011, pia imekuwa ikipambana kuzijumuisha pamoja pande mbili hasimu za jeshi, kuandaa katiba mpya,  na kutayarisha pia uchaguzi wake kwa nza mwezi Desemba mwaka huu.