Yameeandika; Mkutano wa OPEC, vita vya Aleppo na mvutano kati ya Ulaya na Uturuki | Magazetini | DW | 01.12.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazeti ya Ujerumani

Yameeandika; Mkutano wa OPEC, vita vya Aleppo na mvutano kati ya Ulaya na Uturuki

Kutokuchukuliwa hatua na nchi za Magharibi za kuuingilia vita katika mji wa Aleppo kunahatarisha hali jumla ya usalama duniani.

Gazeti la «Stuttgarter Nachrichten»na mgomo wa Lufthansa

Kutokuwepo kwa msimamo wa mariadhiano kwa viongozi wa shirika la Lufthansa kunaweza kukasababisha mustakabali usiokuwa mwema kwa shirika hilo na badala yake kulivuruga kabisa.Viongozi wa wafanyakazi waliotangaza mpango huo wa kulivuruga shirika lao wenyewe  ikiwa wakuu wa shirika hilo hawatoridhia mapendekezo yao, Hata wao wenyewe wanahusika katika mchakato wa kiwango cha mapato cha Ujerumani kinachohusu kazi maalum.Hali hii kwahivyo haileti tena usawa na badala yake imewafanya marubani kuvunjwa moyo kabisa na msimamo wa kiongozi wao Carsten Spohr. Pamoja na kwamba binafsi ni rubani lakini amechukuwa mwelekeo mwingine kabisa na kuwaona marubani wenzie wanataka kujipatia fedha zaidi za mshahara kuliko wafanyakazi wengine wa shirika hilo wanavyopata .

Gazeti la «Rheinpfalz»  kuhusu  Uturuki na Umoja wa Ulaya.

Kansela Angela Merkel amekizungumzia kile ambacho tokea hapo kinajulikana na wengi. Katika hali ambayo inaonesha yanayofanyika Uturuki hayaridhishi bila shaka yoyote kunayaondowa matumaini ya kuendelea mazungumzo ya Uturuki. Hata kauli ya Kansela Merkel inatowa ujumbe wa dhahiri wa ishara  kubwa kuhusu azimio lilopitishwa na bunge la Ulaya ambalo hata hivyo haliziwajibishi kisheria nchi za Umoja huo. Kwa maana hiyo si hasha tukaiona Uturuki kutolizingatia azimio hilo na kulipuuza na kushuhudia tena wimbi la wakimbizi wanaotumia maboti kuingia Ulaya. Kwa hali kama hii  je serikali ya Ujerumani ina mpango wa pili katika kulidhibiti hili?

«Badische Neueste Nachrichten» vita vinavyoendelea Aleppo

Kwa mara nyingine ulimwengu unashuhudia tena kilichowahi kushuhdiwa huko nyuma. Nchi za Magharibi zimebaki kutazama na kushindwa kufanya lolote. Hali hii inaweza kusababisha madhara makubwa katika  mapambano ya umwagaji damu ya kuukomboa mji wa Aleppo kuendelea kwa kipindi cha miongo,Tena sio Aleppo tu lakini duniani kwa Ujumla. Na hii ni kwa sababu kwa upande mmoja viongozi wanahisi wanaweza kukwepa kuchukuliwa hatua na kwa hivyo wana uwezo wa kufanya chochote wanachotaka. Na kwa upande mwingine ni wimbi la Wakimbizi kutoka eneo hilo ambalo kwa sasa ni suala la muda tu.

Gazeti la «Landeszeitung»  juu ya mkutano wa Opec

Kupanda kwa bei ya mafuta kungeweza kuwa ni habari njema ikiwa ukweli huu ungekwenda sambamba na  ugunduzi wa vitalu vingine zaidi vya mafuta ambavyo vimeshuhudiwa kupungua sana katika hali ambayo haijapata kutokea kwa kipindi cha miaka 70. Lingekuwa jambo bora zaidi endapo nchi zilizoendelea kiviwanda zingetambua mapema kwamba bidhaa hii  muhimu ambayo ni kama damu ya dunia itafikia mwisho. Makubaliano kati ya nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi za OPEC ya kupunguza utoaji mafuta yamejifungamanisha na mapambano ya siasa za kieneo. Katika mapambano ambayo Saudi Arabia imeshindwa, kwani baada ya kushikilia msimamo wake wa kuweka ukomo wa uzalishaji mafuta kwa muda mrefu, hatimaye jana iliridhia ongezeko la uchimbaji mafuta ili kuukabili ushindani wa mafuta ghafi kutoka Marekani katika soko na kuzuia kuporomoka kwa bei ya bidhaa hiyo. Saudi Arabia haikufaulu hesabu zake na badala yake kilichodhihirika ni kwamba makampuni yanayopingana na Saudia yameamua kushusha gharama ya uzalishaji kwa hadi asilimia 40 katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu na hivyo kulinda hisa zao.

Mwandishi: Saumu Yusuf

Mhariri: Daniel Gakuba