Wolfsburg inabidi leo kuitimua nje Leverkusen | Michezo | DW | 17.04.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Wolfsburg inabidi leo kuitimua nje Leverkusen

Bundesliga:Leverkusen itaizuia safari ya ubingwa ya Wolfsburg leo ?

Patrick Helms (B.Lev.)

Patrick Helms (B.Lev.)

Baada ya changamoto za Champions League-kombe la klabu bingwa barani Ulaya na kombe la UEFA ambalo limetia timu 2 za Ujerumani katika hatua ya nusui-finali Hamburg na Bremen na 2 za Ukraine, changamoto za Ligi zinarudi uwanjani leo na kesho Jumapili:Katika Bundesliga, macho yanakodolewa mpambano wa leo kati ya viongozi wa Ligi Wolfsburg na timu pekee iliothubutu kuwashinda msimu huu Bayer Leverkusen.Nchini Uingereza, leo ni nusu-finali ya Kombe la FA: Arsenal ina miadi leo na Chelsea.

Wolfsburg, viongozi wa Bundesliga wanabidi kweli kuchunga leo wakitembelewa nyumbani na timu pekee iliowatia munda msimu huu-Bayer Leverkusen.Wiolfsburg ikiongozwa na kocha Felix Magath,imepania kutetea uongozi wake wa pointi 3 kileleni.Leverkliusen sio tu iliizaba Wiolfsburg mabao 2-0 mapema msimu huu,lakini pia ina rekodi nzuri ya kucheza nje katika Bundesliga ,licha ya kuwa iko nafasi ya 9 ya ngazi ya Ligi.

Lakini, ikiwa Leverkusen ina rekodi nzuri nje, Wolfsburg imekuwa ikitamba nyumbani na hivyo, haitaliachia jogoo la shamba kuwika leo mjini Wolfsburg na kuwatungua kutoka kileleni .Wolfsburg, imeshinda mapambano 12 nyumbani na kutoka sare mara 1 katika mapambano yake 13 iliocheza Volkswagen Arena.Isitoshe, hawakushindwa mechi 9 sasa mfululizo n a hii ndio sababu wakitamba na mbrazil Grafeti,wako kileleni mwa Ligi.

Mabingwa Bayern Munich, wako pointi 3 nyuma ya Wolfsburg sawa na Hamburg iliokata tiketi ya nusu-finali ya Kombe la ulaya la UEFA kati ya wiki ilipoipiga kumbo Manchester city .Ushindi chupuchupu wa mabao 2-1 dhidi ya timu iliopo mkiani mwa Ligi Borussia Moenchengladbach,mwishoni mwa wiki iliopita ni mfano wa hatari ya Wolfsburg kuteleza kutoka kileleni.

Angalia Hertha Berlin , ni mfano wa timu iliokua kileleni,lakini kama wasemavyo, "alie juu ,mgoje chini."Mapambano 3 yaliopita,Berlin ikiongoza kwa pointi 4 na kabla changamoto za leo wako pointi 5 nyuma.

Mabingwa Bayern Munich, baada ya kupigwa kumbo nje ya champions league na FC Barcelona, kufuatia pigo la mabao 4-0 na sare ya bao 1-1, sasa wanajua tamaa yao pekee ni kutetea ubibngwa wao nyumbani na kuona wanakata tiketi ya champions league-mwakani.Munich leo, inaitembelea Armenia Bielefeld na inajua kocha wao Klinsmann hamudu kupoteza pointi zaidi,shoka linameta-meta. Stuttgart ilioanza kuja kwa menon ya juu,imejiwinda kulipiza kisasi leo kwa FC Cologne, ilioilaza duru iliopita nyumbani.Hoffenheim, iliopungua kasi ina miadi na Karlsruhe ambayo takriban imeshazama daraja ya pili.

Borussia Dortmund inaitembelea leo Bochum wakati Frankfurt ina kibarua kikubwa kuizima vishindo vya Borussia Moenchengladbach inayotapatapa isizame daraja ya pili. Duru hii ilifunguliwa tayari jana na changamoto kati ya Schalke na Cottbus.

Huko Uingereza, mbali na mpambano wa nusu-final ya kombe la FA kati ya Arsenal na Chelsea, timu nyengine zinaingia uwanjani kwa prem,ier league-Ligi ya uingereza.Aston villa inacheza na West Ham Utd. Middlesbrough inaikaribisha nyumbani FDulham sawa na Portsmouth inayopambana na Bolton Wanderes.Stoke City inacheza na Blackburn Rovers .Sundereland inacheza na Hull City.

Katika la Liga-ligi ya Spian, FC Barcelona ilioitimua Bayern Munich kuingia ili nusu-finali ya champions league, inaitembelea leo Getafe kudai pointi nyengine 3 ili kupanua zaidi mwanya wake kileleni.Mahasimu wao Real Madrid, wanapokewa mikono 2 na Recreativo Huelva wakati Malaga inaahidi kuikomoa Real Mallorca.Atletico Madrid ina miadi leo na Numancia wakati Atletico Bilbao inapanga kuzima vishindo i vya Deportivo la Coruna.

Muandishi: Ramadhan Ali

Mhariri: Saumu Y.Ramadhani