1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Watu 32,226 waeuawa Gaza hadi sasa

Lilian Mtono
24 Machi 2024

Wizara ya Afya ya Ukanda wa Gaza unaoendeshwa na Hamas imesema karibu watu 32,226 wameuawa katika Ukanda huo tangu kuzuka kwa vita kati ya wanamgambo hao na Israel miezi mitano iliyopita.

https://p.dw.com/p/4e4Mm
Mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza
Wapalestina wakiwa wanatizama vifusi baada ya mashambulizi ya usiku kucha ya Israel yaliyoshambulia eneo la kambi ya wakimbizi ya Nuseirat, katikati ya Ukanda wa GazaPicha: AFP

Idadi hiyo inajumuisha karibu vifo 84 vilivyotokea masaa 24 yaliyopita, hii ikiwa ni kulingana na taarifa ya wizara hiyo iliyoongeza kuwa watu 74,518 wamejeruhiwa huko Gaza.

Na huko mjini Tel Aviv,nchini Israel, maelfu ya Waisreali wameandamana jana wakishinikiza kuachiliwa huru mateka wanaoshikiliwa na Hamas, huku wakionyesha kumpinga Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na serikali yake.

Inaarifiwa kuwa waandamanaji hao waliwasha moto kwenye mitaa iliyoko katikati ya jiji hilo na kufunga barabara kuu.

Miito yao ilikuwa dhidi ya Netanyahu ambaye wakosoaji wanasema ameshindwa kudhibiti mgogoro huo tangu mashambulizi ya Hamas kusini mwa Israel mwezi Oktoba mwaka uliopita, yaliyochochea vita.