Winnie Madikizela Mandela afariki dunia | Matukio ya Afrika | DW | 02.04.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Winnie Madikizela Mandela afariki dunia

Mwanaharati huyo wa zamani dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini amefariki (02.04.2018) akiwa na umri wa miaka 81.

Winnie Madikizela Mandela, mwanaharakati dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini na aliyekuwa mke wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela ameaga dunia hii leo. Hayo ni kulingana na msaidizi wake Zodwa Zwane. Bi Mandela amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 81.

Taarifa kutoka kwa familia yake imesema amefariki kwa amani leo mchana akiwa amezingirwa na wapendwa wake katika hospitali moja mjini Johannesburg baada ya kuugua kwa muda mrefu. Taarifa hiyo imeongeza kuwa Winnie amekuwa akilazwa mara kwa mara tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Winnie Mandela ambaye alikuwa mke wa Rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini Nelson Mandela kwa miaka 38 alichangia pakubwa katika kampeini za kukomesha utawala wa ubaguzi wa rangi lakini pia historia yake ilikumbwa na kashfa chungu nzima.

Mwandishi:Caro Robi/rtre/afpe

Mhariri:Sekione Kitojo