1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO yapandisha tahadhari ya hatari ya Ebola nchini Kongo

22 Mei 2026

Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema hatari ya kiafya kwa umma kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeongezwa kwa kiwango cha juu zaidi.

https://p.dw.com/p/5EChA
DR Congo Bunia 2026 | Wahudumu wa Shirika la Msalaba Mwekundu wakiwa wamebeba jeneza la mwathirika wa Ebola
Wahudumu wa Shirika la Msalaba Mwekundu wakiwa wamebeba jeneza la mwathirika wa EbolaPicha: Gradel Muyisa Mumbere/REUTERS

Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema hatari ya kiafya kwa umma kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeongezwa kwa kiwango cha juu zaidi.

Hata hivyo, Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema kuwa, kiwango cha hatari kinasalia kuwa cha juu katika ngazi ya kikanda na cha chini katika ngazi ya dunia. Alitoa kauli hiyo Ijumaa katika mkutano na wanahabari.

Kwa mujibu wa WHO, kwa sasa kuna karibu visa 750 vinavyoshukiwa kuwa vya Ebola nchini Kongo, huku vifo vinavyohusishwa na ugonjwa huo vikifikia 177.

Wakati huo pia hofu imezidi kutanda baada ya mlipuko wa Ebola kuenea hadi jimbo la Kivu Kusini mashariki mwa Congo eneo linalodhibitiwa na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda.