1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO yaonya ongezeko la maambukizi ya magonjwa ya zinaa

Sylvia Mwehozi
22 Mei 2024

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, jumla ya watu zaidi ya milioni 1 huambukizwa magonjwa ya zinaa kila siku ikiwemo kaswende na kisonono. Ongezeko kubwa zaidi la maambukizi limeshuhudiwa barani Amerika na Afrika.

https://p.dw.com/p/4g7rb
Tedros Adhanom Ghebreyesus
Tedros Adhanom Ghebreyesus mkurugenzi wa WHOPicha: Ajit Solanki/AP/dpa/picture alliance

Shirika la Afya Duniani WHO limetoa tahadhari kuhusu changamoto katika mapambano dhidi ya magonjwa ya zinaa. Kulingana na taarifa ya iliyotolewa na WHO, idadi ya kila mwaka ya maambukizi mapya ya ugonjwa wa kaswende iliongezeka kutoka karibu milioni 7.1 mwaka 2020 hadi milioni 8 mwaka 2022.

Jumla ya watu 230,000 walikufa kutokana na magonjwa ya bakteria mwaka 2022. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, jumla ya watu zaidi ya milioni 1 huambukizwa magonjwa ya zinaa kila siku ikiwemo kaswende na kisonono.

Ripoti hiyo pia ilihusia kupungua polepole kwa maambukizi mapya ya VVU. WHO inasema nchi nyingi tayari zimeendeleza mikakati ya kiafya ya kuzuia maambukizi ya VVU na kaswende kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.