WHO: COVID-19 upo mbali na kumalizika | Matukio ya Kisiasa | DW | 30.06.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

WHO: COVID-19 upo mbali na kumalizika

WHO: COVID-19 upo mbali na kumalizika

Shirika la Afya Duniani, WHO limeonya kwamba janga la virusi vya corona hata halipo karibu kumalizika, katika kipindi ambacho idadi ya vifo ulimwenguni kote ikipindukia nusu milioni.

Maeneo yaliothirika zaidi kwa sasa ni mataifa ya Amerika ya Kusini na Marekani. Na katika hatua nyingine idadi ya walioathirika duniani kote ikifikia watu milioni 10, huku baadhi ya serikali hatua za kudhibiti maambukizi ambazo zimeathiri uchumi wa dunia. Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus anasema "Tunataka jambo hili lifikie mwisho. Sote tunahitaji maisha yetu."

Lakini aliongeza kwa kusema kwamba ukweli mchungu kwamba janga hilo halipo karibuni na kumalizika, ingawa mataifa mengi yamepata mafanikio, lakini kwa uhalisia kimataifa janga hilo limeongeza kasi yake.

WHO kuchunguza kiini cha virusi vya corona China

Brasilien Coronavirus | Ausbruch in Sao Paulo

Wachimba makaburi wa mjini Sao Paulo, Brazil

Hata hivyo, Tedros amesema juma lijalo WHO, itapeleka ujumbe wake China, ambako ugonjwa huo ulizuka miezi sita iliyopita kwa lengo la kutafuta kiini chake. COVID-19 bado inaathiri kwa kasi katika maeneo ya Marekani, ambako kumerekodiwa  vifo zaidi ya 125,000 na maambukizi milioni 2.5. Makadirio hayo yanaweza kufikia robo ya maambukizi yote ulimwenguni.

Afisa mwandamizi wa serikali ya Marekani, Jerome Powell amesema katika kipindi cha Aprili-Juni kulitarajiwa kunyong'onyea kwa pato la ndani GDP, na kuongeza kwamba ukarabati wa hali hiyo utategemea jitihda za serikali katika udhibiti wa mripuko wa virusi vya corona. Majimbo mengi ya kusini na magharibi ya Marekani, ambayo yameathiriwa vibaya na virusi, viongozi wake wamelazimika kufungua shughuli za kawaida mapema.

Soma zaidi:Merkel na Macron kuujadili mpango wa uokozi wa corona

Na wakati chama cha upinzani cha Democrat, kikimtaka Trump kutoa maazimio ya dharura kuhusu virusi vya corona, Afisa habari mwandamizi wa Ikulu ya White House mjini Washington Kayleigh McEnany amesema rais hana mpango huo.

Brazil, kama taifa linaloshika nafasi ya pili kwa maamnukizi kwa wakati huu limeorodhesha maambukizi 259,105. Huko Ireland watu wamejitokeza kwa wingi katika vilabu vya pombe baada ya majuma 15 ya marufuku ya kukabiliana na virusi. Ulaya, bado ni eneo lililoathiriwa vibaya ingawa nchi zimeendelea kufunguliwa huku kukiripotiwa visa vipya.