1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

White House: Hatuna taarifa za mashambulizi ya Rafah

16 Machi 2024

Msemaji wa Baraza la Usalama la Taifa nchini Marekani John Kirby amesema bado hawajaarifiwa juu ya operesheni ya kijeshi katika mji wa Rafah.

https://p.dw.com/p/4dnI8
Israel-Hamas-Krieg | Israelischer Luftangriff in der Nähe eines UNRWA-Lagerhauses in Rafah
Wapalestina wakiomboleza kwenye mwili wa mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa aliyeuawa katika shambulizi la anga la Israel karibu na ghala la Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA).Picha: Abed Rahim Khatib/dpa/picture alliance

Marekani imesema hayo ikiwa ni saa chache baada ya ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kusema kuwa imetia saini mipango ya operesheni hiyo ya kijeshi.

Kirby amewaambia waandishi wa habari katika Ikulu ya White House kwamba Marekani haitaunga mkono mpango huo bila ya mapendekezo "ya kuaminika" ya kuwalinda raia wa Gaza.

Zaidi ya watu milioni 1.5 wanajihifadhi katika mji huo wa kusini mwa Gaza, na washirika wa Israel kama Marekani wameonya dhidi ya operesheni ya haraka ya kijeshi katika mji huo ili kuwaondoa wapiganaji waliosalia wa Hamas walioko huko.

Rais wa Marekani Joe Biden amesema, kwa upande wake anaona uvamizi wa Rafah utavuka "mstari mwekundu" ikiwa hakutakuwa na mipango ya kuaminika ya kuwalinda raia.

Huku hayo yakiendelea, Meli ya kwanza ya chakula cha msaada iliyotokea Cyprus hadi Gaza jana Ijumaa imeanza kupakua shehena ya chakula katika eneo hilo la Palestina lililozingirwa.