1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSlovakia

Waziri Mkuu wa Slovakia afanyiwa upasuaji mwingine

18 Mei 2024

Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico amefanyiwa upasuaji mwingine siku ya Ijumaa.

https://p.dw.com/p/4g1NI
Wahudumu wa afya wakimuwahisha kupatiwa matibabu Waziri Mkuu wa Slovakia
Wahudumu wa afya wakimuwahisha kupatiwa matibabu Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico baada ya kushambuliwa kwa risasi: 15.05.2024Picha: Jan Kroslak/TASR via AP/picture alliance

Upasuaji huo umefanyika ikiwa ni siku mbili baada ya kupigwa risasi tumboni. Maafisa wanasema baada ya upasuaji huo, hali ya mwanasiasa huyo bado si ya kuridhisha.

Serikali mjini Bratislava imesema taarifa zaidi juu ya hali ya Waziri Fico itawekwa wazi "wakati hali itakaporuhusu." Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis amemuandikia barua rais wa Slovakia Zuzana Caputová, na  kulaani kitendo hicho huku akimtakia ahueni kiongozi huyo.

Mshukiwa wa tukio hilo ambaye inasemekana ni mzee mwenye umri wa miaka 71 anashikiliwa na Polisi. Hata hivyo waendesha mashitaka wamezitaka mamlaka za usalama kutotoa maelezo zaidi kuhusu kesi hiyo.