Waziri Mkuu wa Mali akataa kujiuzulu | Matukio ya Afrika | DW | 31.07.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Waziri Mkuu wa Mali akataa kujiuzulu

Waziri Mkuu wa Mali,Boubou Cissé,amekataa pendekezo la upinzani la kutaka ajiuzulu na kusema kwamba mzozo wa nchi hiyo utapatiwa ufumbuzi kupitia mazungumzo.

Kujiuzulu kwangu hakuko kwenye ajenda,asema Boubou Cissé waziri mkuu wa Mali.

Kujiuzulu kwangu hakuko kwenye ajenda,asema Boubou Cissé waziri mkuu wa Mali.

Waziri mkuu wa Mali,Boubou Cissé amekataa pendekezo la upinzani la kutaka ajiuzulu  na kusema kwamba mzozo wa nchi hiyo utapatiwa ufumbuzi kupitia mazungumzo. Kwenye mahojiano makhsusi na DW,Cissé amesema vuguvugu la maandamano nchini mwake linatakiwa kushiriki kwenye serikali ya muungano.

Madai ya upinzani ya kutaka kujiuzulu kwa rais Ibrahim Keita na waziri mkuu wake, yamegonga mwamba. Waziri mkuu wa Mali Boubou Cissé anasema kujiuzulu kwao sio suluhisho la mzozo huo wa kisiasa.

''Kujiuzulu kwangu hakuko kwenye ajenda.Ni Rais pekee alienamamlaka hayo, ya kuteuwa waziri mkuu na endapo haridhishwi,kumtaka ajiuzulu.Tunamaelewano mazuri na Rais na mtizamo wetu wa pamoja ni kuwepo na suluhisho la mzozo huu''.

Muungano wa kundi la  vuguvu la M5-RFP linaloandaa maandamano nchini Mali umeitisha hatua nyingine zaidi za wananchi kutotii sheria za nchi.Ulamaa Mahmoud Dicko,mwenye ushawishi mkubwa kwenye vuguvugu hilo la maandamano alisema kujiuzulu kwa waziri mku pekee hakuwezi kuutatuwa mkwamo wa kisiasa uliopo,bali kunaweza kuwa sehemu ya muafaka.

''Watu napita na taifa litabaki daima''

Alipoulizwa endapo upinzani utakata kushiriki kwenye serikali ya muungano, waziri mkuu Cissé anasema hakuwezi kuzuwiya mageuzi yanayopangwa kufanyika.

''Niya yetu na kwangu binafsi ni kwamba ni lazima tufikie maridhiano ya pamoja na upinzani.Lakini ikiwa hawatokubali basi nchi haiwezi kusimama. Watu wanapita na taita litabaki daima,kwa hiyo tutafanya kazi na watu watakaokubali kutuunga mkono katika kujenga taifa letu''.

Mali imekumbwa na maandamano ambayo yameitikisa serikali tangu mwezi Juni na yamesababisha hofu za kiusalama.

Mali imekumbwa na maandamano ambayo yameitikisa serikali tangu mwezi Juni na yamesababisha hofu za kiusalama.

Kuhusu pendekezo la viongozi wa jumuiya ya ECOWAS la kutaka kujiuzulu kwa kundi la wabunge ambalo linalalamikiwa na wapinzani kuingia bungeni kupitia wizi wa kura.Waziri mkuu  Boubou Cissé anasema madai yote ya upinzani yanajadiliwa na baadhi yatapatiwa ufumbuzi kupitia mazungumzo.

Wabunge wakaidi azmio la ECOWAS

Tayari kiongozi wa wabunge hao 31, Gougan Coulibaly, amesema kwamba hawatajiuzulu kwa kuwa pendekezo hilo la ECOWAS linakwenda kinyume na katiba ya Mali.

Kwenye mkutano wa kilele kwa njia ya vidio hapo jumatatu, viongozi wakuu wa nchi 15 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Magharibi ya Afrika (ECOWAS) walisema wanamuunga mkono Rais Keita lakini wakatoa wito wa kuundwa serikali ya pamoja itakayojumuisha upande wa upinzani.Jumuiya ya ECOWAS vile vile ililitaka bunge la Mali kujiuzulu ifikapo leo ijumaa ya Julai 31 na kuruhusu kuitishwa uchaguzi mpya.

Mali imekumbwa na maandamano ambayo yameitikisa serikali tangu mwezi Juni na yamesababisha hofu ya kuvuruga jitihada za kupambana na makundi ya Waislamu wenye itikadi kali katika mataifa ya magharibi mwa Afrika.