1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Burundi yatahadharisha juu ya usalama wa chanjo

Amida Issa18 Oktoba 2021

Guillaume Bunyoni ametahadharisha umma juu ya usalama wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Covid 19,akisema Burundi ililazimika kuipokea kufuatia shinikizo za wafadhali.

https://p.dw.com/p/41p4h
Kenia Impfung Dadaab Flüchtlingslager
Picha: Getty Images

Akihutubia wakaazi wa Tarafani Mbiga Kayowe mkoani Rutana alikopeleka misaada kwa watu maskini, Waziri Mkuu Alain Guillaume Bunyoni amesema kuwa serikali haina uhakika juu ya usalama wa chanjo ya Covid 19 na kwamba haifahamu iwapo chanjo hiyo itakuwa na madhara au la kwa watu watakaopewa chanjo hiyo.

Bunyoni amesema baada ya serikali kupokea shehena ya kwanza ya chanjo hiyo, kumeibuka maswali mengi kutoka kwa raia juu ya usalama wa chanjo yenyewe.

Bunyoni ameweka wazi kuwa chanjo ya Covid-19 inatolewa kwa hiyari na kuwa haibebi dhamana juu ya madhara yanaoweza kutokea kwa mtu aliyepokea chanjo.

"Tulipata chanjo nyingi tangu tulipo kuwa watoto za kutukinga dhidi ya maradhi mbali mbali, lakini ni tafauti kabisa na chanjo hii ya Covid 19. Imekuwa chanjo ya kwanza kugunduliwa haraka haraka, wataalam waloigunduwa hawakupata muda wa kuthmini madhara yake.'' alisema Bunyoni kabla ya kuendelea  ''Baadhi wanazungmza kisiri siri, Na ndio sababu unapo nunuwa aidha unapo pigwa chanjo hiyo unatakiwa kusaini waraka wa kubali kuma madhara yake hayako kwenye jukumu la walotengeneza chanjo hiyo."

Soma pia:Burundi yamtuhumu kiongozi wa upinzani kwa 'vitendo vya kigaidi'

''Raia atakaye taka kupata chanjo yuko huru''

Waziri Mkuu wa Burundi Alain Guillaume Bunyoni (kulia) na rais wake Evariste Ndayishimiye.
Waziri Mkuu wa Burundi Alain Guillaume Bunyoni (kulia) na rais wake Evariste Ndayishimiye.

Waziri mkuu Alain Guillaume Bunyoni pia ameonyesha wasiwasi wake juu ya aina nyingi za chanjo ya Covid-19 kinyume na mfumo wa zamani ambapo kulikuwa na chanjo moja pekee inayokubaliwa na shirika la afya duniani.

"Chanjo dhidi ya Covid 19 zimekuwa nyingi, takribani kutoka kila nchi yenye uwezo imekuwa ikitengeneza chanjo yake. Nchi imezipokea chanjo hizo kufuatia shinikizo za wafadhili.  Raia atakaye taka kupata chanjo yuko huru, lakini mwatakiwa kujuwa wapo walopata chanjo na baadaye kuambukiwa na Covid 19 na wengine walikufa."alisema Bunyoni.

Waziri mkuu huyo amesema isitoshe chanjo dhidi ya Covid 19 ni bei ghali, na kubaini kuwa shehena ya chanjo laki 5 iliopokea Burundi  kutoka China ina thamani ya takribani milioni 3 dola za marekeni Na kuuliza endapo Burundi itahitaji chanjo kwa raia wake zaidi ya milioni 10 itagharimu kiasi gani cha fedha.

Soma pia:Hali ya COVID 19 ikoje mpakani mwa Burundi na Tanzania?

Idadi ndogo ya visa vya maambukizi vya Covid-19

Bunyoni amewatolea mwito wananchi kuzingatia kanuni za wizara ya afya katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona na kusisitiza kuwa hio ndio njia pekee itakayowaletea ufanisi.

Burundi imeripoti idadi ndogo ya vifo na wagonjwa wa Covid-19 ukilinganisha na nchi nyingine za kanda hii.

Baada ya kupokea wiki jana shehena ya kwanza ya chanjo dhidi ya Covid 19 kutoka china, Burundi inataraji kupokea mwezi Novemba shehena nyingine zaidi ya milioni 2 kutoka shirika la afya duniani.