1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu zaidi wauwawa katika mapigano Yemen

Sudi Mnette
30 Julai 2018

Mapigano makali yanayoendelea katika eneo la pwani ya mashariki ya Yemen kati ya wapiganaji wanaoiunga mkono serikali na waaasi wa Kishia yamesababisha vifo vya idadi kubwa ya watu kwa pande zote hasimu.

https://p.dw.com/p/32Iho
Jemen Krieg - Taez
Picha: Getty Images/AFP/A. Al-Basha

Hayo yanatokea katika kipindi ambacho watumishi katika sekta ya afya wakiripoti kasi ya mripuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika maeneo kadhaa ya taifa hilo. Sudi Mnette anaarifu zaidi

Jeshi la serikali, lenye kuungwa mkono na muungano unaoongozwa na Saudi Arabia yanasonga mbele kwa wiki za hivi karibuni katika maeneo ambayo wanakabiliana na waasi wa kihouthi wanaoungwa mkono na Iran . Mapigano hayo yanatajwa kushika kasi katika kipindi ambacho majeshi ya serikali yakijaribu kuidhibiti upya bandari ya Hodeida, bandari muhimu kwa kuingiza vyakula katika taifa hilo ambalo linaelekia katika kubiliwa na baa la njaa.

Maafisa wa serikali imekuwa ikifanya mashambulizi ya kuiwezesha kuitekea wilaya inayodhibitiwa na waasi ya Zabid. Wanasema mapigano yanaendeshwa na wanajeshi wa ardhini wenye silaha kali huku wakisaidiwa na mashambulizi ya angani. Mapigano hayo ya kuudhibiti mji huo, moja ya eneo la turathi la UNESCO, ambayo yamesababisha idadi kubwa ya watu kupoteza maisha kwa hivi sasa yameingia mwaka wake wa nne.

Watu 18 wauwawa ad-Durayhimi

Jemen Krieg l Wassernot in Sana
Adha ya maji kwa wakazi wa SanaaPicha: picture-alliance/RIA Novosti

Habari kutoka kwa maafisa na watu wengine walioshuhudia zinasema mashambulizi ya Jumapili katika wilaya ya ad-Durayhimi, kusini mwa Hodeida yamesababisha vifo vya watu 18. Waasi wa Houthi walikuwa wakijaribu kuingia katika eneo hilo, wakiwa umbali wa kilometa 20 kusini mwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hodeida.

Mratibu wa masuala ya kiutu wa Umoja wa Mataifa Lise Grande amesema mashambulizi ya angani yameharibu mifumo ya maji taka mjini Zabid pomoja na mfumo wa usambazaji maji safi amabo unahudumia pia idadi kubwa ya watu katika mji wa Hodeida. Amesema mashambulizi hayo kwa ujumla yanawaweka raia katika hali ya hatari sana. Nae Youssef Al-Hadhery, msemaji wa wizara ya afya anasema alizungumzia athari za mashambulizi alisema "Pamoja na kuanza kwa msimu wa kiangazi na mvua na ongezeko la mashumbulizi ya majeshi ya muungano katika maeneo ya miradi na miundombinu ambayo inasaidia kudhibiti kusambaa kwa kipindupindu, kama miradi ya maji safi ya kunywa na mifumo ya maji taka, na mingine, pamoja na kulengwa kwa hospitali na kuendeleza mzingiro. Hayo yamesababisha kuwepo kwa kiwango kikubwa cha kipindupindu na sasa tunashuhudia mripuko mpya ambao unaweza kuwa mbaya zaidi kuliko wa awali."

Katika muendelezo wa matokeo mabaya ya mapigano nchini Yemen, maafisa wa usalama wa taifa hilo wamesema watu walikuwa na silaha wamemuuwa kwa kumpiga risasi afisa mwandamizi wa usalama wa taifa hilo katika eneo la kusini mwa mji wqa bandari wa Aden. Duru zinaeleza Kanali Nasser Makrij aliuwawa Jana Jumapili wakati akiwa anatembea kwa miguu karibu na nyumbani kwake mjini Aden.

Tangu mwaka 2015, serikali ya Yemen ikiungwa mkono na majeshi ya muuungano yanayoongozwa na Saudi Arabia yanashiriki operesheni za kivita dhidi ya waasi wa Kishia ambao pia wanajulikana kama Houthi, ambao wanaudhibiti mji mkuu wa Sanaa, na sehemu kubwa ya kaskazini mwa Yemen.

Mwandishi: Sudi Mnette APE

Mhariri: Saumu Yusuf