1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu kadhaa waliuwawa DRC mnamo mwezi Septemba

Sekione Kitojo
1 Novemba 2018

Makundi yenye silaha pamoja na majeshi ya usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamefanya mauaji ya watu 92 mwezi  Septemba.

https://p.dw.com/p/37VWM
Picha ya maktaba
Picha ya maktabaPicha: AP

Ofisi ya kutetea  haki  za  binadamu  ya  Umoja  wa Mataifa  imesema  makundi  yenye  silaha  pamoja  na majeshi  ya  usalama  katika  Jamhuri  ya  Kidemokrasi  ya Congo  wamefanya  mauaji  ya  watu  92 mwezi  Septemba.

Ofisi  ya pamoja  ya  Umoja  wa  mataifa  kwa  ajili  ya haki  za  binadamu  imerekodi  matukio 623  ya  ukiukaji wa  haki  za  binadamu katika  nchi  hiyo kubwa  ya Afrika  ya  kati  mwezi  uliopita , ikiwa  ni  ongezeko  kutoka matukio  620  mwezi  Agosti   na  matukio  515  mwezi Julai.

Ofisi  hiyo  imeongeza  kwamba  asilimia  48  imefanywa  na wapiganaji  kutoka  makundi  ya  watu  wenye  silaha, ikiwa ni  pamoja  na  mauaji  ya  kiasi  watu 67.