Watu bilioni moja kupewa chanjo ya homa ya manjano Afrika | NRS-Import | DW | 12.04.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

NRS-Import

Watu bilioni moja kupewa chanjo ya homa ya manjano Afrika

Umoja wa Mataifa utaendesha kampeni ya kutoa chanjo dhidi ya homa ya manjano barani Afrika. Kampeni hiyo inalenga watu bilioni moja ifikapo 2026

Takriban watu bilioni moja barani Afrika watapewa chanjo dhidi ya homa ya manjano ifikapo mwaka 2026 katika kampeni inayoendeshwa na Umoja wa Mataifa yenye lengo la kutokomeza homa hiyo barani Afrika.

Virusi vinavyosababisha homa ya manjano vinavyosambazwa na mbu huuawa watu wengi barani humo na husambaa haraka katika maeneo yanayokaliwa na watu wengi.

Akizindua kampeni hiyo ya chanjo nchini Nigeria, Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema sindano moja tu ya chanjo hiyo ya kinga dhidi ya homa ya manjano itamlinda mtu dhidi ya ugonjwa huo kabisa.

Nigeria hivi sasa inakabiliwa na mripuko wa homa ya manjano huku mamia ya watu wakiripotiwa kuathirika tangu mwezi Agosti. Nusu ya idadi ya waathiriwa ni watoto.Miongoni mwa nchi zinazotajwa na WHO kuwa katika hatari kubwa ya kuwa na mripuko wa homa ya manjano ni Sudan, Sudan Kusini, Uganda na Jmahuri ya kidemokrasia ya Congo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com