1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 7 wameuawa katika shambulio la kikabila nchini Pakistan

9 Mei 2024

Watu wenye silaha kusini-magharibi mwa Pakistan wamewaua watu saba wakiwa usingizini, katika kile polisi wanakiita kuwa ni tukio la pili la ugaidi wa kikabila katika eneo hilohilo ndani ya mwezi mmoja.

https://p.dw.com/p/4fg8Q
Pakistan | Jengo la hospital ambako miili ya waliuwawa inahifadhiwa
Jengo la hospital nchini Pakistan ambako miili ya waliuwawa inahifadhiwaPicha: Abdul Ghani Kakar/DW

Shambulio hilo limefanyika katika mji tete wa Pwani wa Gwadar ambako mshirika wa kisiasa wa Pakistan China inajenga bandari ya kina kirefu cha bahari, mradi unaopingwa na nchi za Magharibi.

Mkuu wa jeshi la polisi katika eneo hilo, Mohsin Ali amesema walikuwa wakazi wa jimbo la kati la Punjab na kujishghulisha na biashara ya unyozi wa nywele.

Soma pia:Iran na Pakistan kuimarisha uhusiano wao wa kibiashara na kiusalama

Hilo ni tukio la pili kuwalenga watu kutoka Punjab katika eneo hilo  la jimbo la Balochistan ambalo linakabiliwa na mashambulizi ya wanamgambo kwa takriban majuma matatu sasa.