1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAustralia

Watu kadhaa wauawa kwenye shambulizi la kisu mjini Sydney

Lilian Mtono
14 Aprili 2024

Raia mmoja wa Pakistan ametajwa kuwa miongoni mwa watu waliouawa katika shambulizi la kisu kwenye mtaa wenye shughuli nyingi za manunuzi mjini Sydney.

https://p.dw.com/p/4eju1
Sydney | Shambulio la kisu
Afisa wa Polisi na yule wa huduma ya dharura wakiwa katita eneo la tukio ambapo watu kadhaa wameuawa katika shambulio la kisu mjini Sydney:13.04.2024Picha: Steven Saphore/AP Photo/picture alliance

Kulingana na Jumuiya ya Kitaifa ya Wapakistani nchini Australia na Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya, raia huyo aliyefahamika kwa jina la Faraz Tahir aliuliwa na mshambuliaji aliyekuwa na kisu, ambaye pia aliwaua wanawake watano.

Jumuiya hizo zimefanya maombolezo ya kijana huyo waliyesema alihamia Australia mwaka uliopita. Jumuiya ya Wapakistani imeiomba jamii kusimama pamoja na familia za wahanga na waliowapoteza wapendwa wao.

Polisi imemtaja mshambuliaji kuwa ni Joel Cauchi ambaye wamesema aliwahi kukutwa na matatizo ya afya ya akili.